SIRI YA MTUMIAJI
Kila Shirikisho la Afya ya Akili Duniani, Eli Lilly and Company na Boehringer Ingelheim inaheshimu siri ya wageni wa tovuti zao, kama matokeo yake, tumeanzisha sera ya siri ya tovuti hii. Sera ya siri ya tovuti hii inatumika tu kwa utendakazi wa tovuti ambazo zinaungana moja kwa moja na sera hii unapobonyeza "taarifa ya siri” kwenye wayo wa tovuti.
Kupitia tovuti hii Shirikisho la Afya ya Akili Duniani, Lilly na Boehringer Ingelheim itakusanya habari ambazo zinaweza kukutambulisha, kama vile jina lako, anwani, namba ya simu, barua pepe, anwani, na habari zingine kama hizo (“Habari Zako”) wakati tunapopewa kwa hiari (walakini, angalia mjadala hapo chini kuhusu “Anwani za IP” ikiwa una unganisho wa bendipana (broadband)). Tutatumia Habari Zako kujibu maswali unayo kutuhusu sisi, na mara kwa mara, tunaweza kurejelea habari zako ili tuweze kufahamu mahitaji yako vyema na vile tunavyoweza kuboresha tovuti, bidhaa na huduma zetu. Pia tunaweza kutumia habari Zako kuwasiliana na wewe au kukupatia habari za kijumla za afya (kama vile habari juu ya hali zingine za afya) na hata pia habari kuhusu bidhaa na huduma zetu. Pia tunaweza kuboresha au kuunganisha Habari Zako na data zilizopokewa kutoka kwa mtu wa tatu kwa madhumuni hayo hayo.
Habari zingine zozote zilizohalalishwa na wewe zinazohusiana na wewe kutembelea tovuti hii (“Habari Zingine” – yaani, habari ambazo haziwezi kutumiwa kukutambua) zinaweza kujumuishwa katika hifadhidata inayomilikiwa na kukimiwa na Shirikisho la Afya ya Akili Duniani, Lilly na Boehringer au maajenti wake. Shirikisho la Afya ya Akili Duniani, Lilly na Boehringer Ingelheim hubakia na haki zote za hifadhidata hii na habari zilizomo ndani yake. Habari zingine tunazokusanya zinaweza kujumuisha Anwani ya IP na habari zingine zilizokusanywa kupitia kumbukumbu za wavu na kuki (angalia hapo chini).
Tovuti hii inaweza kutumia teknolojia inayojulikana kama violeza vya wavu – wakati mwingine huitwa single-pixel gifs – ambazo huruhusu tovuti hii kukusanya habari za kumbukumbu ya wavu. Kioleza cha wavu ni mchoro kwenye ukurasa wa wavu au katika ujumbe wa barua pepe iliyoundwa ili kufuata kurasa zilizoangaliwa au ujumbe uliofunguliwa. Habari ya kumbukumbu ya wavu hukusanywa wakati unapotembelea mojawapo ya tovuti zetu na kompyuta inayosimamia tovuti yetu (inayoitwa "Seva ya wavu”). Seva hii ya wavu hutambua yenyewe habari zingine zisizo za kibinafsi, kama vile tarehe na saa uliyotembelea tovuti yetu, kurasa ulizotembelea, tovuti uliyotoka, aina ya kivinjari unachotumia (k.v., Internet Explorer), aina ya mfumo wa utendakazi unaotumia (k.v., Windows 2000), na jina la kikoa na anwani ya mtoa huduma wako ya Wavuti (k.v., AOL). Pia tunaweza kujumuisha violeza vya wavu katika ujumbe wa barua pepe ya matangazo ili kujua kama ujumbe umefunguliwa.
Tovuti hii inaweza kutumia teknolojia iitwayo "kuki". Kuki ni kipande cha habari ambacho seva yetu ya wavu hutuma kwa kompyuta yako (kwa faili yako ya kivinjari) unapofikia tovuti yetu. Kisha wakati unaporudi tena tovuti yetu itajua una mojawapo ya kuki zetu kwenye kompyuta yako. Kuki zetu husaidia kutoa kazi zaidi kwa tovuti na hutusaidia sisi kuchunguza utumiaji wa tovuti kwa usahihi zaidi. Kwa mfano, tovuti yetu inaweza kuweka kuki kwenye kivinjari chako ambacho hufanya usihitaji kukumbuka na kuingiza nywila yako zaidi ya mara moja wakati unapotembelea tovuti hii.
Tovuti hii hutumia anwani za Itifaki ya Wavuti (IP). Anwani ya IP ni namba iliyopangiwa kompyuta yako na Mtoa huduma wako ya Wavuti ili uweze kufikia wavuti. Kwa ujumla, anwani ya IP hubadilika kila wakati unapounganisha wavuti (ni anwani "badilifu"). Kumbuka, walakini kwamba, ikiwa una unganisho wa bendipana, ikitegemea na hali yako ya kibinafsi, inawezekana kwamba anwani yako ya IP ambayo tunakusanya, au pengine kuki tunayotumia, inaweza kujumuisha habari ambazo zinaweza kuonekana zinatumika. Hii ni kwa sababu unganisho zingine za bendipana, anwani yako ya IP haibadiliki (ni “tuli’) na inaweza kuhusishwa na kompyuta yako ya kibinafsi. Sisi hutumia anwani yako ya IP kuripoti habari za mkusanyiko zinazotumika na kujaribu kuboresha tovuti hii.
Unapaswa kufahamu kwamba tovuti hii haijakusudiwa, au kuundwa ili kuvutia watu walio chini ya umri wa miaka 18. Hatukusanyi habari za kibinafsi zinazotambulika kutoka kwa mtu yeyote ambaye kwa kweli tunajua yuko chini ya umri wa miaka 18.
Maeneo ya tovuti hii ambayo inakusanya Habari Zako hutumia kiwango cha tasnia cha usimbaji fiche wa safu ya soketi salama (SSL); walakini, ili uweze kuchukua fursa hii, kivinjari chako lazima kikubali ulinzi wa usimbaji fiche (unaopatikana katika Internet Explorer toleo la 3.0 na kuendelea).
Tunaweza kushiriki habari Zako na maajenti, makontrakta au washirika wa Shirikisho la Afya ya Akili Duniani, Lilly na Boehringer Ingelheim kuhusiana na huduma ambazo watu hawa au vyombo hivi vinafanya na Shirikisho la Afya ya Akili Duniani, Lilly na Boehringer Ingelheim. Maajenti hawa, makontrakta au washirika wamekatazwa kutumia data hizi kwa njia yoyote ile isipokuwa kutoa huduma kwa Shirikisho la Afya Ya Akili Duniani, Lilly na Boehringer Ingelheim, au huduma kwa ushirikiano ambao wao na Shirikisho la Afya ya Akili Duniani, Lilly na Boehringer Ingelheim wanahusika (kwa mfano, baadhi ya bidhaa zetu hukuzwa na kuuzwa kupitia makubaliano ya pamoja na makampuni mengine). Tunaweza, kwa mfano, kutoa habari zako kwa maajenti, makontrakta, au washirika kwa kuhudumia hifadhidata yetu, kwa huduma za kuchakata data, au ili waweze kukutumia habari ulizouliza.
Shirikisho la Afya ya Akili Duniani, Lilly na Boehringer Ingelheim huhifadhi haki ya kushiriki habari Zako ili kujibu utawala wa serikali au inapohitajika na sheria maombi ya habari zilizoidhinishwa. Katika hali nadra sana ambapo usalama wa taifa, jimbo au kampuni unahusika (kama vile kitendo cha ughaidi cha Kituo cha Biashara Duniani mnamo Septemba, 2001), Shirikisho la Afya ya Akili Duniani, Lilly na Boehringer Ingelheim huhifadhi haki ya kushiriki hifadhidata yetu yote ya wageni na wateja na utawala wa serikali unaofaa.
Pia tunaweza kutoa Habari zako zinazohusiana na mauzo, kazi, au hawalisho zingine za biashara ya tovuti ambayo inahusiana na habari hii kwa mtu wa tatu, katika hali hiyo tutahitaji mnunuzi kama huyo kukubali kushughulikia Habari Zako kulingana na Sera ya Siri.
Kama urahisishaji kwa wageni wetu, Tovuti hii kwa sasa ina viungo vya tovuti kadhaa ambavyo tunaamini vinaweza kutoa habari muhimu. Sera na utaratibu tuliofafanua hapa hautumiki kwa tovuti hizo. Tunapendekeza kuwasiliana na tovuti hizo kwa habari juu ya siri, usalama, ukusanyaji data, na usambazaji wa sera zao.
Ili kuondolewa kutoka kwa orodha ya mawasiliano, tafadhali andikia Lilly kwa anwani inayofuata:
Eli Lilly and Company
P.O. Box 6245
Indianapolis, IN 46206-6245
United States of America
Tafadhali pia kumbuka kwamba kujiondoa kutoka kwa orodha ya mawasiliano hakutakuondoa kutoka kwa orodha yoyote iliyoanzishwa kupitia tovuti yoyote ile inayokimiwa na Shirikisho la Afya ya Akili Duniani au Boehringer Ingelheim.
Tafadhali kumbuka kwamba unaweza kuendelea kupokea taarifa tunapoendelea kusasisha orodha zetu.
Tunaweza kusasisha Sera ya Siri ya Tovuti hii mara kwa mara. Wakatu tunapoisasisha, kwa urahisi wako, tutafanya sera iliyosasishwa ipatikane kwenye ukurasa huu.
Ilisasishwa Mwisho: Oct. 25, 2006
