Kusonga Kuelekea Ahueni

Unyogovu ni zaidi ya kuhisi "kutochangamka", na siyo ishara ya udhaifu wa nafsi. Ni ugonjwa wa kawaida, wa hatari na mgumu kufahamika ambao huathiri takriban watu milioni 121 ulimwenguni kote 1.

Ijapokuwa watu walio na unyogovu wana matatizo ya kununa, kama vile kupoteza tamaa au furaha, mara kwa mara hao huelezea hali zao kwa matatizo ya afya ya mwili. Hali hiyo ikiwachwa bila kutibiwa, inaweza kusababisha matatizo ya mahusiano, pamoja na matatizo ya kindoa na ya familia, matatizo ya kikazi na hatari kubwa ya kujiua2,3.

Mapato kutoka kwa utafiti wa kimataifa uliotekelezwa mapema mwaka wa 2005 kwa niaba ya Shirikisho la Afya ya Akili Duniani (World Federation for Mental Health) (WFMH) lilifichua mapengo thabiti katika ufahamu wa wagonjwa' na madaktari kuhusu unyogovu, iliyosababisha utambuzi mbaya au utambuzi uliyocheleweshwa.4 Kwa mfano, watu wanaosumbuliwa na unyogovu, kwa kadri, walisubiri zaidi ya miezi 11 ili kumwona daktari na walitambuliwa wana unyogovu baada ya kumtembelea daktari mara tano, hiyo ilichelewesha zaidi matibabu na ahueni. 4

Breaking Through Barriers ilianzishwa ili kuwasaidia watu walio na unyogovu, familia zao na marafiki kujifunza zaidi kuhusu unyogovu - sababu zake, dalili, madhara na chaguzi za kimatibabu - na hufanya kazi kwa ushirikiano, pamoja na watoa huduma ya matibabu, ili kuvunja vizuizi vya ahueni.

Rejeleo
  1. World Health Organization. Factsheet - Depression. 2005. Inapatikana kwa http://www.who.int/mental_health/management/depression/definition/en/
  2. Pincus HA, Pettit AR. J Clin Psychiatry. 2001;62(suppl 6):5-9.3095-3105
  3. Bradvik L, Berglund M. Late mortality in severe depression. Acad Psychiatry Scand. 2001;103:111-116
  4. 'Depression: The Painful Truth' Survey. . Iliyofanywa na Harris Interactive kati ya Februari 21 na Aprili 11, 2005. Inapatikana kwa: http://www.wfmh.org/PainfulTruthsurvey.htm