Kupanga mpango wa kupona
Kupanga mpango wa kupona
Mojawapo ya mambo mazuri unayoweza kufanya ni kumsaidia Mwenza wako kufafanua na kufikia malengo yake ya kupona kama sehemu ya mpango wake wa kupona. Himizo lako na mafunzo ni muhimu kwa mpango huu kufaulu.
Kwa kuongezea kutafuta matibabu kutoka kwa taalamu wa huduma ya afya, ni muhimu kwako na kwa Mwenza wako kupitia mazoezi yafuatayo:
- Fafanua malengo ( ikiwa kuweka lengo kumeidhinishwa na mtoa huduma ya afya).
- Tatambua vielelezo au matukio maalumu ambayo yanaweza kusababisha unyogovu kuendelea zaidi.
- Buni mbinu ambazo zinaweza kutumiwa kupita ugonjwa huo.
- Tengeneza orodha ya ishara za mapema ambazo zinaweza kumaanisha unyogovu umerudi.
Kufuata maendeleo
Kwa mtu ambaye ana unyogovu, inawezakuwa vigumu kutambua maendeleo ya kila siku ambayo inaonyesha anaendelea kupata nafuu. Msaidie Mwenza wako kutambua kwamba anapata nafuu; wacha mwenza wako ajue kwamba unatambua kwamba malengo yanafikiwa, na msherehekee mafanikio haya pamoja. Ita kila ishara ya kuendelea, haijalishi vile ni ndogo, kwa kusema mambo kama:
- “Sijakusikia ukicheka hivyo sana kwa muda mrefu.”
- “Siku hizi unaonekana umetulia sana.”
- “Umeanza kulima bustani tena.”
- “Unaonekana unashughulika zaidi na miradi kazini.”
Weka akilini kwamba inaweza kukuhuzunisha ikiwa malengo ya Mwenza wako hayafikiwi kwa haraka. Zingatia malengo madogo kwanza na usubiri kushughulikia malengo makubwa hadi ajihisi vyema. Mwenza wako anaweza kukasirika, kwa hivyo angalia mazungumzo yoyote mabaya kumuhusu. Hii inaweza kupunguza maendeleo, na unapaswa umtie moyo Mwenza wako ajaribu kuepukana nayo. Unapokuwa ukipitia vitengo vya unyogovu na Mwenza wako, weka akilini kwamba kila mtu upitia unyogovu (na kupona) vitofauti, na mahitaji yake yanaweza kubadilika baada ya muda. Ili kufuata mabadiliko haya, endelea kuwasiliana.
Uhusiano kati ya unyogovu na kujiua
Kama mtu anayejali kuhusu mtu aliye na unyogovu, ni muhimu kwamba uelewe uhusiano kati ya unyogovu na kujiua. Siyo watu wote walio na unyogovu wana mawazo ya kujiua, na si kila wazo la kujiua linasababisha kujiua, lakini kujiua kunakohusiana na unyogovu ni wa kweli. Jaribu usiruhusu uwoga wa kukabiliana na ugumu huu ukushushe moyo wa kusaidia. Ili kuamua kama mtu ana mawazo ya kujiua, jaribu kuuliza:
- “Je! unafikiria kuhusu kujiumiza?”
- “Je! unafikiria kuhusu kufa moyo?”
- “Je! Unahitaji usaidizi wa kujilinda?”
Ikiwa jibu lake ni “ndiyo” kwa mojawapo ya maswali haya, ni muhimu umsaidie Mwenza wako kutafuta usaidizi wa mtaalamu mara moja. Lazima Mwenza wako ampigie simu daktari wake mara moja. Ikiwa Mwenza wako hawezi kupiga simu hii, unapaswa kuwasiliana na mtaalamu wa huduma ya afya.
Ijapokuwa utatulia ikiwa majibu ya maswali yako kuhusu kujiua ni “hapana” unapaswa kufahamu kwamba wakati wote wa ugonjwa huo, dalili za mtu zinaweza kuzidi na kwamba anawezakuwa na mawazo ya kujiua.. Endelea kuangalia dalili hizi na hata pia wasiwasi, fadhaa, hofu, ugumu wa kulala, kuwashwa, uhasama, uchokozi, mihemko, kutotulia, au kufurahi kupita kiasi na kuhangaika. Ikiwa moja kati ya mabadiliko haya ni kali au hufanyika kwa ghafula, inaweza kuonyesha hatari iliyoongezeka ya wazo au tabia yaa kujiua. Kuwa na uhakika haswa kwamba Mwenza wako anaripoti dalili zozote wakati anapoanza tiba ya madawa ya unyogovu na wakati wowote kuna mabadiliko katika kipimo.
Jijali
Kumsaidia mtu ambaye ana ugonjwa wa hatari kama vile unyogovu inaweza kuwa vigumu sana. Ijapokuwa kuna uwezekano mkubwa Mwenza wako ataanza kuhisi vizuri na matibabu, unaweza kupata kwamba mambo yanaendelea polepole mara ya kwanza. Pirikapirika za kuishi na unyogovu zinaweza kukuhemesha, hata pia Mwenza wako, kwa hivyo ni muhimu ujijali. Hakikisha umejijali ili uweze kumsaidia Mwenzako.
Kama Mwenza Msaidizi, wewe ni wa dhamana kwa rafiki yako au mpendwa wako ambaye anangangana na unyogovu. Umechagua kuchukua kazi muhimu. Inawezakuwa safari ndefu kwenye wote, lakini usaidizi wako unawezakuwa kifunguo cha Mwenzako kupona na aweza kufurahiya maisha tele.
