Breaking Through Barriers hulenga kusaidia kuhakikisha kwamba watu walio na unyogovu wanaosumbuliwa na dalili za mhemko na za kimwili wametambuliwa na kutibiwa vizuri kama iwezekanavyo Information for Support Partners- Breaking Through Barriers hulenga kusaidia kuhakikisha kwamba watu walio na unyogovu wanaosumbuliwa na dalili za mhemko na za kimwili wametambuliwa na kutibiwa vizuri kama iwezekanavyo

Mpango wa usaidizi

Hatua ya kwanza ni kuuliza Mwenza wako kuhusu aina ya usaidizi unaohitaji. Mara ya kwanza, Mwenza wako anawezakuwa hajui, au anawezakuwa hataki kukuambia. Usikufe moyo. Badala yake, toa mifano maalum ya vile unavyoweza kutoa usaidizi wa mhemko na wa kazi:

Usaidizi wa mhemko

Usaidizi wa kikazi

Kwa kuwa sasa unajua mahitaji ya Mwenza, hatua inayofuata ni kuweka mpangilio wako mwenyewe. Kwa mfano, kujikabidhi kupiga simu kila jioni ili kuzungumza au kuwachukua watoto kutoka kwa mazoezi ya mpira. Kwa kuchuja hitaji la Mwenza wako kuuliza usaidizi kila mara, utamsaidia kuzingatia kujihisi vyema.

Kuweka malengo ya usoni

Mwenza wako akitambua usaidizi wa kikazi kama hitaji, hakikisha kwamba usaidizi wako haujeleweshi kupata nafuu kwa Mwenza wako. Ijapokuwa Mwenza wako atathamini usaidizi wako, kuchukua majukumu yake mengi hakutamsaidia Mwenza wako mwishowe. Kumbuka, jukumu lako kama Mwenza Msaidizi ni kumtia moyo na kumsaidia. Chukua kila nafasi kujenga uwezo wa Mwenza wako kwa kumtia moyo achukue hatua. Kwa mfano, ikiwa umejikabidhi kupika chakula cha jioni cha Mwenza wako kila Alhamisi, unaweza kuamua kwamba “kupika pamoja” inapaswa kuwa lengo la muda mrefu. Mwangalie Mwenza wako mara kwa mara kuhusu uwezo wake na umtie moyo kila wakati ili afikie malengo yake ya kila hatua njiani.

Panga kikundi cha Wenza Wasaidizi

Ikiwa Mwenza wako anaishi na unyogovu wa hatari, anaweza kuhitaji usaidizi zaidi ya ule unaoweza kutoa. Wewe na Mwenza wako mnastahili mjadiliane kuhusu kuunda kikundi cha Wenza Wasaidizi. Ukihisi hii inaweza kufanyakazi, zungumza na Mwenza wako ili uhakikishe kwamba yuko sawa na kuhusisha watu wengine. Baada ya kukubaliana kuhusisha wengine, Mwenza wako anastahili kwanza kuwatambua washirika wengine. Kikundi kinapaswa kuwasiliana mara kwa mara kuhusu vile nyinyi wote mnaweza kufanyakazi kwa pamoja na kugawana majukumu.