Chaguzi za matibabu
Tiba ya kuzungumza
Kuna aina nyingi za taaluma na tiba ya magonjwa ya akili na matibabu, au “tiba ya kuzungumza,” ambayo inaweza kumsaidia mtu aliye na unyogovu kuelewa ni nini inayosababisha hali hiyo. Aina mbili za kawaida za taaluma na tiba ya magonjwa ya akili inayotumiwa katika unyogovu wa hatari ni:
- Utabibu wa utambuzi wa kitabia — huzingatia kubadilisha mawazo na tabia mbaya ambayo inaweza kusababisha unyogovu.
- Utabibu kati ya watu wawili — huzingatia kuchunguza masuala ya uhusiano na wengine ili kutambua shida na kubadilisha tabia
Watu wengine walio na unyogovu pia wanaweza kufaidika kutoka kwa tiba ya watu wawili, tiba ya familia au tiba ya kikundi (vipindi ambavyo watu walio na ugonjwa sawa hufanya kazi kwa pamoja na mtaalamu aliyefunzwa). Kuna tiba ya kuzungumza ya aina nyingi, inaweza kuchukua majaribio chache ya kumpata mtaalamu au tiba ambayo “inafaa”, lakini hiyo ni sawa, na siyo jambo lisilo la kawaida. Jambo la maana ni kupata matibabu ambayo yatafanyakazi vyema kwa mahitaji ya mtu.
Madawa ya Unyogovu (Antidepressants)
Inaaminika kwamba unyogovu unawezakuwa unasababishwa na kutokuwa sawa kwa kemikali zinazopatikana ndani ya ubongo na mwilini iitwayo vipitisha neva. Madawa ya unyogovu kwa kawaida hupangwa kulingana na vile zinavyofanya kazi, ijapokuwa madawa mpya yanapagwa kulingana na athari zake za kuzuia uchukuaji tena wa vipitishaji tofauti vya neva ndani ya ubongo na mwilini, haswa norepinephrine (NE), serotonin (5-HT) na dopamine (DA)1.
Mambo mengi yanaweza kuathiri chaguo la madawa ya unyogovu: Uzuri wake, usalama, athari, hali ya sasa ya madawa na hali ya akili, gharama, urahisi wa kutumia, utumiaji na kama madawa mengine yanatumiwa.
Madawa ya Unyogovu kwa kawaida huchukua wiki mbili hadi nne ili kuanza kufanya kazi2. ikiwa hakuna maendeleo yoyote au kidogo iliyogunduliwa baada ya wiki nne hadi nane, daktari anaweza kuamua kubadilisha kipimo cha madawa au anaweza kuongeza au kubadilisha na madawa mengine ya unyogovu1. Wataalamu wa tiba na magonjwa ya akili kwa kawaida hupendekeza kwamba watu walio na unyogovu waendelee kutumia madawa kwa miezi mitano au zaidi baada ya dalili kuwa nzuri ili kupunguza uwezekano wa kurudi tena. Mtaalamu wa huduma ya afya anapaswa kumfuatilia mtu anayetumia madawa ya unyogovu ili aone vile anavyokubali matibabu. Daktari atakuwa akiangalia kipimo na kujua kama ni nzuri kwa kutibu dalili zote – za mhemko na za kimwili. Mtaalamu wa huduma ya afya atafafanua athari zinazoweza kutokea, ambayo ya kawaida sana inaweza kujumuisha kichefuchefu, kukauka mdogo, usingizi, hamu kupungua na kutoa jasho jingi. Athari zozote zisizotarajiwa zinapaswa kuripotiwa moja kwa moja kwa mtaalamu wa huduma ya afya.
Wakati mtu ana unyogovu, kunawezakuwa na dalili zake zinaweza kuzidi au ana mawazo ya kujiua. Mabadiliko yoyote yasiyo ya kawaida ya kitabia, ikijumuisha wasiwasi, fadhaa, hofu, ugumu wa kulala, kuwashwa, uhasama, uchokozi, mihemko, kutotulia, au kufurahi kupita kiasi na kuhangaika inapaswa kuripotiwa kwa daktari mara moja. Ikiwa moja kati ya mabadiliko haya ni kali au hufanyika kwa ghafula, inaweza kumaanisha kwamba kuna hatari kubwa ya wazo au tabia ya kujiua. Pia, kuwa mwangalifu sana uripoti dalili yoyote wakati wa kuanza tiba yoyote ya madawa ya unyogovu na wakati wowote kuna mabadiliko katika kipimo. S
Vikundi vya usaidizi
Hakuna yeyote aliye na unyogovu anastahili kujihisi mpweke. Vikundi vya usaidizi ni mahali ambapo watu walio na unyogovu na wale ambao wanawajali wanaweza kushiriki masaibu yao, kujadili njia za kuvumilia unyogovu na kutoa tumaini wenyewe kwa wenyewe.
Pia, vikundi vya usaidizi huwatia moyo watu walio na unyogovu kufuata mpango wao wa matibabu na kuwasaidia kuelewa kwamba matatizo ya mhemko haikufafanui wewe ni nani. Kwa kuongezea, vikundi vya usaidizi hutoa baraza la kukubali sawa, kuelewa na kujijua mwenyewe. Lakini ni muhimu kukumbuka kwamba vikundi vya usaidizi si ubadilisho wa huduma ya mtaalamu. Vikundi vingi vya usaidizi havikubali au kupendekeza utumiaji wa matibabu au madawa maalumu.
Unaweza kupata vikundi vya usaidizi vilivyo karibu na wewe kwa kuwasilian na vikundi vyoyote vya uteteaji vilivyoorodheshwa chini ya Rasilimali na Viungo.
Afya na Maslahi
Wakati mtu ana unyogovu, kuzingatia kuboresha afya na maslahi pia inaweza kusaidia. Mazoezi na lishe iliyoboreshwa inaweza kuwasaidia watu kuhisi vyema na katika hali zingine pia kuboresha hali ya kiroho inaweza kuwa ya manufaa.
Rejeleo
- Blier P. Crosstalk between the norepinephrine and serotonin systems and its role in the antidepressant response. J Psychiatry Neurosci. 2001;26 Suppl:S3-10.
- Delgado P, Approaches to the Enhancement of Patient Adherence to Antidepressant Medication Treatment. J Clin Psychiatry 2000;61 (suppl2)
