Kuanza urafiki
Kupata maneno “sawa” ya kutoa usaidizi wako inaweza kuwa vigumu kwa watu wengi. Iwe mtu unayemjali ametambuliwa, au unadhania mpendwa wako anawezakuwa na unyogovu, kuanza mazungumzo hakustahili kuwa ni vigumu au ya kuaibisha. Kwa hakika, unaweza kushangazwa kupata kwamba mtu huyo ametulia kwa kuwa mwishowe anaweza kumwambia mtu siri.
Tayari, .... anza kuzungumza! !
Unapokuwa ukijadili unyogovu, jambo muhimu la mazungumzo mazuri ni kuonyesha kujali kwako na huruma bila ya kuhukumu. Epuka kuonyesha makosa ya zamani ya mtu unapoanza mjadala; pia, hepuka lugha mbaya. Badala yake, zingatie njia hizi ikiwa mtu tayari amekuambia kuhusu utambuzi wake:
- “Nimekuwa nikiangalia unyogovu baada ya kusema kwamba ilitambuliwa, na ukiamua unahitaji usaidizi, haupaswi kuipitia peke yako.”
- “Je! Mtoa huduma wako ya afya amependekeza uweke malengo fulani? Ikiwa ni hivyo, ninaweza kufanyakazi na wewe ili kuanzisha mpango ambao utakusaidia urejee kujihisi vyema?”
- Ni vyema kwamba mtaalamu wako wa huduma ya afya ameagiza matibabu ya unyogovu wako, lakini ni vipi kuhusu vitu vidogo-vidogo ambavyo bado vinakufadhahisha? Niko hapa ikiwa unahitaji chochote.”
- “Ikiwa unyogovu wako unafanya kufanya vitu kuwa vigumu, wakati zamani ilikuwa ni rahisi, niko hapa ili kukusaidia na chochote unachohitaji.”
Unachostahili kusema ikiwa unashuku rafiki au mshirika wa familia ana unyogovu:
- “Je! Umegundua siku hizi hauko sawa? Je! Umefikiria kuhusu kwenda kumuona mtaalamu wa matibabu? Ninaweza kwenda na wewe, ikiwa una wasiwasi.”
- “Je! Unadhania mtaalamu wa huduma ya afya ataweza kukusaidia ujihisi tena vyema? Unaweza kuniruhusu nikusaidia kutafuta mmoja?”
- “Inaonekana kana kwamba umekuwa na wakati mgumu siku hizi. Je! umefikiria kuhusu kutafuta usaidizi wa mtaalamu? Haustahili kupitia suala hili kivyako.”
Ikiwa mara ya kwanza haufanikiwi
Watu wengi huona ni vigumu kukubali usaidizi. Toleo lako linaweza kukataliwa kwa sababu nyingi — aibu, kukosa kuelewa kuhusu unyogovu, hisia za kutokuwa na dhamana au uwoga wa kupoteza uhuru. Hii ikifanyika, usiwe na wasiwasi. Wakati haujafika wa kukubali usaidizi. Usisitize wakati huo. Badala yake, sisitiza baadaye kwa upole. Katika hali hii, jambo muhimu ni kwamba umuhimize mtu huyo kutafuta usaidizi au aendelee kumwona wa huduma ya afya.
