Breaking Through Barriers hulenga kusaidia kuhakikisha kwamba watu walio na unyogovu wanaosumbuliwa na dalili za mhemko na za kimwili wametambuliwa na kutibiwa vizuri kama iwezekanavyo Information for Support Partners- Breaking Through Barriers hulenga kusaidia kuhakikisha kwamba watu walio na unyogovu wanaosumbuliwa na dalili za mhemko na za kimwili wametambuliwa na kutibiwa vizuri kama iwezekanavyo

Kujikabidhi

Kwa sababu ni vigumu kumwangalia mtu unayemjali akingangana na unyogovu, hisia yako ya kwanza ni kuingilia na kutatua vitu. Ijapokuwa hii inaeleweka, siyo njia nzuri ya kusaidia ya kuanza nayo. Kusikia nafuu ya kweli itachukua muda na inaweza kuhusisha vikwazo kadhaa, kwa hivyo unahitaji kwanza kufikiria kiwango cha kujikabidhi unachoweza. Habari hii itakusaidia kuweka vizuizi, kumsaidia Mwenza wako kujua anachostahili kutarajia, na itajenga msingi dhabiti wa kufaulu. Ikiwa unahisi hauna wakati mwingi wa kujitolea, au ikiwa maisha yako au kazi inakuzuia kutokana na kuhusika kama utakavyo, hiyo ni sawa. Wakati mwingine kuwepo ili kuzungumza mara moja kwa muda ni usaidizi wa kutosha. Kumbuka, kiwango chochote cha usaidizi kimekaribishwa.

Amua muda wako wa kujikabidhi

Kabla ya kumkaribia mtu aliye na unyogovu ili kumpatia usaidizi, zingatia ifwatayo:

Ikiwa unaishi na mtu aliye na unyogovu, swali si kama una muda wa kujikabidhi, bali unaweza kusaidia aje. Ni muhimu kufikiria kuhusu kuelewa unyogovu na vile inavyoathiri uhusiano wako. Kwa kufanya hivi, utaelewa vyema maeneo ambayo anaweza kuhitaji usaidizi zaidi.

Kujua uwezo wako

Kutoa usaidizi kwa mtu aliye na unyogovu hakustahili kuchukua muda wako wote. Watu wengine wanaweza kuhitaji usaidizi wa kushughulikia mambo ya kila siku ya maisha, wakati wengine wanaweza kuhitaji rafiki wa kumsaidia kuegemea kihisia. Haijalishi ni kazi gani — kubwa au ndogo — usaidizi wako unaweza kupunguza hisia za kutengwa, ili kuhisi vyema kuonekane kuko karibu.

Kabla ya kusaidia, unastahili kuelewa uwezo wako na upungufu wako. Kwa mfano,
Ikiwa una utu wa kuchukua husukani kwa nguvu, kutoweza “kutatua” mambo kwa haraka kunaweza kukutatanisha. Kwa hivyo, unaweza kuhitaji kuzingatia kusaidia kwa njia ambazo zinafaa zaidi. Tumia utu wako kumsaidia Mwenza wako na kazi za kila siku kama vile kununua mboga au kuwachukua watoto kutoka shuleni. Ikiwa wewe ni mtatua shida, unaweza kufaa zaidi kumsaidia mwenza wako kujaza fomu za bima na kumsaidia kuelewa zinasimamia nini. Au, pengine, wewe ni mzuri kwa kusikiliza – unawezakuwa msaidizi wa ajabu wa kihisia kwa mpendwa wako. Unaweza kutumia mifano hii ili kukusaidia kutengeneza orodha ya ustadi wako mwenyewe, na vile inaweza kutumiwa vyema.