Breaking Through Barriers hulenga kusaidia kuhakikisha kwamba watu walio na unyogovu wanaosumbuliwa na dalili za mhemko na za kimwili wametambuliwa na kutibiwa vizuri kama iwezekanavyo Information for Support Partners- Breaking Through Barriers hulenga kusaidia kuhakikisha kwamba watu walio na unyogovu wanaosumbuliwa na dalili za mhemko na za kimwili wametambuliwa na kutibiwa vizuri kama iwezekanavyo

Unyogovu – ugonjwa uliyoenea na uliyoeleweka vibaya

Kuenea

Unyogovu ni wa kawaida sana ulimwengu kote, na unaongezeka:

Sababu

Bado sababu ya unyogovu haujaeleweka vyema na, kwa kweli, wakati mwingine kunaweza kuwa na sababu zinazoweza kuonekana. Wataalamu wanaamini watu wengine walizaliwa na uwezo wa kupata unyogovu kwa urahisi4. Pia, wanaamini kwamba matukio ya kufadhaisha, ugonjwa, madawa na mambo mengine yanaweza kusababisha kutokuwa sawa kwa kemikali zingine za ubongo na kusababisha unyogovu5.

Watu wengine wanapata unyogovu baada ya mabadiliko makubwa ya maisha – kifo cha mtu unayempenda, talaka, kupoteza kazi au kuhama. Hata matukio ya furaha, kama vile kuwa mzazi au kufunga ndoa, au mabadiliko madogo maishani, wakati mwingine yanaweza kuleta unyogovu. Haijalishi ukubwa au udogo wa mabadiliko maishani, mabadiliko yanaweza kuwa ya kufadhaisha na yanaweza kuathiri pakubwa hisia za mtu.

Baadhi ya mambo ya hatari ya unyogovu ni pamoja na:

Unyogovu unaweza kusababishwa na hali zingine za kimatibabu. Magonjwa kama vile kupooza, shtuko la moyo, kansa, ugonjwa wa neva ( kama vile ugonjwa wa kichaa na wa kutetemeka), na mabadiliko ya homoni (kama vile kukatisha hedhi) yanaweza kusababisha unyogovu. Watu walio na hali hizi wanastahili kufahamu haswa dalili za unyogovu na wanapaswa kuzungumza na mtaalamu wao wa huduma ya afya wakihisi mojawapo ya hayo yote.

Unyogovu na kujiua

Kunaweza kuwa na wakati ambao hisia za kutokuwa na matumaini na kupoteza moyo zinaweza kuwasababisha watu walio na unyogovu kufikiria kuhusu kujiua wenyewe. Ukigundua dalili zinazidi kwa mpendwa aliye na unyogovu, kama vile mabadliko yasiyo ya kawaida ya tabia yake, au wasiwasi, fadhaa, mishtuko ya hofu, ugumu wa kulala, kuwashwa, uhasama, uchokozi, mihemko, kutotulia, au kufurahi kupita kiasi na kuhangaika, unapaswa kumhimiza amwone daktari mara moja.

Rejeleo

  1. World Health Organization. Factsheet - Depression. 2005. Inapatikana kwa: http://www.who.int/mental_health/management/depression/definition/en/
  2. WHO. Mental health in the WHO European Region. Fact sheet Euro/03/03. 8 September 2003. Inapatikana kwa: http://www.euro.who.int/document/mediacentre/fs0303e.pdf
  3. World health Organization. Facts sheet. 2002. http://www.who.int/whr/2001/chapter2/en/index4.html
  4. Beardslee WR, Gladstone TRG et al. A Family-Based Approach to the Prevention of Depressive Symptoms in Children at Risk: Evidence of Parental and Child Change. Pediatrics: Official Journal of the American Academy of Pediatrics.2006; 129
  5. Ohayon, MM, Schatzberg, AF. Using Chronic Pain to Predict Depressive Morbidity in the General Population. Arch Gen Psychiatry/Vol 60. 2003: 39