Breaking Through Barriers hulenga kusaidia kuhakikisha kwamba watu walio na unyogovu wanaosumbuliwa na dalili za mhemko na za kimwili wametambuliwa na kutibiwa vizuri kama iwezekanavyo Information for people with depression- Breaking Through Barriers hulenga kusaidia kuhakikisha kwamba watu walio na unyogovu wanaosumbuliwa na dalili za mhemko na za kimwili wametambuliwa na kutibiwa vizuri kama iwezekanavyo

Rasilimali na Viungo

Vikundi vinavyofuata ni mashiriki ya msaada ambayo hutoa habari na usaidizi wa unyogovu na hali zingine zinazohusiana na unyogovu. Ikiwa una maswali maalum kuhusu unyogovu, wasiliana na mojawapo ya vikundi vilivyoorodheshwa hapa ambavyo viko katika nchi yako; vinaweza kukupeleka kwa mashirika mengine ambayo yanawezakuwa na habari maalum unayohitaji.

Viungo vya mashirika

Mashirika ya Australia

Jina: beyondblue

Tovuti: http://www.beyondblue.org.au/

Kuihusu: beyondblue ni shirika la kitaifa, linalojitegemea, liliso la faida linalofanyakazi ili kushughulikia masuala yanayohusiana na unyogovu, wasiwasi na matatizo ya kutumia vibaya vitu vinavyolingana nchini Australia.

Mashirika ya Brazili

Jina: ABRATA

Tovuti: http://www.abrata.com.br

Kuihusu: ABRATA ni shirika ambalo linalenga kuboresha ubora wa maisha kwa watu wanaosumbuliwa na Unyogovu na Ugonjwa wa Kuhuzunika au Kufurahi kupita kiasi (Bipolar), shirika hili halilengi kukomesha mateso yao tu bali pia ya watu wale wanaowasaidia.

Mashirika ya Hispania

Jina: Alianza para la Depresiyon

Tovuti: http://alianzadepresion.com/

Kuihusu: Alianza para la Depresiyon ni shirika la Hispania linalojitegemea, ambalo linatoa ushauri kwa watu walio na unyogovu na familia zao kuhusu jinsi ya kushughulikia unyogovu na kupanga mijadala ya vikundi na mikutano.

Mashirika ya Ufaransa

Jina: Association France Dépressiyon

Tovuti: http://francedepression.free.fr/presentation.htm

Kuihusu: Tovuti ambayo inalenga kutoa usaidizi kwa wagonjwa ili waweze kujihisi hawajatengwa sana na kukataliwa na jamii.


Mashirika ya Italia

Jina: Associazione Strade

Tovuti: http://www.strade-onlus.it/

Kuihusu: Associazione Strade ni shirika la Italia lisilo la kifaida, linakuza utafiti na uzuiaji wa unyogovu. Shirika hili pia linasaidia jamii na marafiki wa watu wanaosumbuka na shida hii.


Mashirika ya Ujerumani

Jina: Bundesverband der Angehörigen psychisch Kranker (BApK)

Tovuti: http://www.bapk.de/

Kuihusu: Bundesverband der Angehörigen psychisch Kranker (BApK) hutoa usaidizi kwa watu walio na unyogovu na jamaa wao kwa kushiriki elimu na kwa kukuza ufahamu wa unyogovu.


Mashirika ya Meksiko

Jina: Voz Pro Salud Mental

Tovuti: http://portal.vozprosaludmental.org.mx

Kuihusu: Tovuti inayotoa habari kuhusu shida hiyo kwa wanaosumbuka na afya ya akili na marafiki wao na familia.

Mashirika Mengine

Jina: Center for Mental Health Services (CMHS)

Tovuti: http://www.mentalhealth.samhsa.gov/

Kuihusu: Usimamiza wa Huduma za Afya ya Akili na Utumiaji Mbaya wa Vitu (SAMHSA) hutoa habari kuhusu afya ya akili kupitia laini ya simu, tovuti na zaidi ya vitabu 600

Jina: The Carter Center

Tovuti: http://www.cartercenter.org/

Kuihusu: Kituo cha Carter kinashirikiana na Chuo Kikuu cha Emory ili kuboresha haki za wanadamu na kukomesha mateso yasiyostahili ya wanadamu. Mpango wa Kituo cha Carter wa Afya ya Akili huzingatia kufanyakazi na vyombo vya habari li kupunguza shutuma na kukuza uandishi mzuri wa habari juu ya matatizo ya afya ya akili.

Jina: Clifford Beers Foundation

Tovuti: http://www.cliffordbeersfoundation.co.uk/

Kuihusu: Kituo cha Carter kinashirikiana na Chuo Kikuu cha Emory ili kuboresha haki za wanadamu na kukomesha mateso yasiyostahili ya wanadamu. Mpango wa Kituo cha Carter wa Afya ya Akili huzingatia kufanyakazi na vyombo vya habari li kupunguza shutuma na kukuza uandishi mzuri wa habari juu ya matatizo ya afya ya akili.

Jina: Depressiyon and Bipolar Support Alliance (DBSA) (US)

Tovuti: http://dbsalliance.org

Kuihusu: The Depressiyon and Bipolar Support Alliance (DBSA) ndilo shirika linaloongoza la kitaifa linalosimamiwa na wagonjwa ambalo linazingatia magonjwa ya akili yaliyoenea – unyogovu na ugonjwa wa kuhuzunika au kufurahi kupita kiasi (Bipolar). Shirika hili ukuza ufahamu kuhusu athari na usimamizi wa magonjwa haya ya kutishia maisha kwa kutoa vifaa vipya vya kisayansi na habari iliyoandikwa katika lugha ambayo umma inaweza kuelewa.

Jina: European Depressiyon Association

Tovuti: http://www.eddas.org/

Kuihusu: Shirika la Unyogovu Uropa (EDA) liliundwa na lengo nzito la kukuza ufahamu wa Unyogovu katika kiwango cha Uropa kupitia kampeni ya kila mwaka ya siku ya Unyogovu Uropa. Kila nchi husika ina mwakilishi ambaye anampa katibu wa Siku ya Unyogovu Uropa katika kiwango cha mtaani, anayekuza kampeni katika nchi yao na kuwaandikisha washauri kwa kamati ya ushauri wa kisayansi. Kanuni kuu nyuma ya EDA ni kwamba kupitia kufanyakazi kwa kushirikiana wanaweza kutumia kabisa rasilimali, kufanyakazi kwa kutumia mbinu, kushawishi vizuri, na kuunda mazingara mema kwa wale ambao wanasumbuliwa na unyogovu.

Jina: Families for Depressiyon Awareness Organization

Tovuti: http://www.familyaware.org/

Kuihusu: Familia za Shirika la Kufahamisha kuhusu Unyogovu liliundwa ili kusaidia familia kutambua na kustahimili matatizo ya unyogovu. Linalenga kusaidia familia kugundua na kusimamia unyogovu na matatizo ya mhemko zinazolingana, kupunguza shutuma inayohusiana na matatizo ya unyogovu na kuunganisha familia na kuzisaidia katika kuvumilia unyogovu huo.

Jina: Gateway to Post Traumatic Stress Disorder

Tovuti:  http://www.ptsdinfo.org/

Kuihusu: Habari ya Matatizo ya Dhiki ya Kiwewe iliundwa ili kusaidia umma kujifunza zaidi kuhusu kuvumilia dhiki ya kiwewe.

Jina: Gift From Within - PTSD Resources

Tovuti: http://www.giftfromwithin.org/

Kuihusu: Tovuti ya kuwapatia walioponea kiwewe, wapendwa wao na wasaidizi tovuti ya mkondoni inayoaminika ambayo ni ya kirafiki na inayosaidia, ambayo itatoa ufafanuzi wa PTSD ambayo si ngumu sana au ya kijuu-juu.

Jina: Health Research Board

Tovuti: http://www.hrb.ie/

Kuihusu: Kamati ya Utafiti wa Afya hulenga kuboresha afya kupitia utafiti na habari.

Jina: Helpguide

Tovuti:  http://www.helpguide.org/index.htm

Kuihusu:   Tovuti hii hulenga kusaidia kuwapa watu nguvu kwa kuwaongoza kuelekea kwa habari inayofaa na kujali shida na mahitaji yao.

Jina: International Centre on Migration and Health (ICMH) 

Tovuti:   http://www.icmh.ch/index.htm

Kuihusu:   Kituo cha Kimataifa cha Uhamiaji na Afya kinaamini kwamba kwa kukuza na kulinda afya na maslahi ya watu wanaoathiriwa na uhamiaji pamoja na watu wanaohama, watu ambao wamewaacha nyuma na jamii zinazowadhamini wahamiaji, afya na maendeleo ya jamii kwa jumla inashughulikiwa vyema.

Jina: International Association of Suicide Prevention

Tovuti: http://www.med.uio.no/iasp/index.html

Kuihusu: ISAP imejitolea kuzuia tabia ya kujiua, kugandamiza athari zake, na kupeana baraza la wasomi, wataalamu wa afya ya akili, wafanyakazi wa wakati wa shida na walioponea kujiua.

Jina: Life Long Mental Health Project

Tovuti: http://www.lifelongmentalhealth.com/index.html

Kuihusu: Tovuti ya kutoa habari juu ya kusimamia afya ya akili ya watu na imegawanywa kwa vikundi 4 vya umri; umri wa miaka 0-4 , umri wa miaka 5-11, umri wa miaka 12-19 na umri wa miaka 20+ .

Jina: Menninger Clinic

Tovuti: http://www.menningerclinic.com/

Kuihusu: Menninger ni kituo cha kimataifa cha ubora cha tiba ya akili, kinarejesha tumaini kwa kila mtu kupitia mipango bunifu ya tiba, utafiti na elimu.

Jina: Mental Health Europe

Tovuti: http://www.mhe-sme.org/

Kuihusu: MHE ni shirika liliso la kiserikali lililojitolea kukuza afya njema ya akili, uzuiaji wa matatizo ya akili, uboreshaji wa huduma, uteteaji na kulinda haki za wanadamu wanaotumia huduma ya afya ya akili, wagonjwa wa hospitali za akili, familia zao na watoa huduma.

Jina: National Alliance for the Mentally Ill (NAMI)

Tovuti: http://www.nami.org

Kuihusu: NAMI (Mwungano wa Kitaifa wa Wagonjwa wa Akili) ni shirika kubwa kabisa la kitaifa la mashinani la afya ya akili lililojitolea kuboresha maisha ya watu wanoishi na shida kubwa ya akili na familia zao. Iiliyoanzishwa mwaka wa 1979, NAMI limekuwa sauti ya taifa juu ya ungonjwa wa akili, shirika la kitaifa ikijumuisha mashirika ya NAMI katika kila jimbo na kwa zaidi ya jamii za mitaa 1,100 nchini kote ambao wanajiunga pamoja kufikia misheni ya NAMI kupitia uteteaji, utafiti, usaidizi na elimu.

Jina: National Institute of Mental Health (NIMH)

Tovuti: http://www.nimh.nih.gov/

Kuihusu: NIMH inahusika sana katika kupanga mbinu na kuweka kipaumbele cha Taasisi nzima na hata pia maeneo maalumu ya utafiti. NIMH hutafuta usaidizi kutoka kwa wagonjwa na mawakili wao, wanasayansi, bunge, umma, na Baraza la Kitafa la Ushauri wa Afya ya Akili.

Jina: National Mental Health Association (NMHA)

Tovuti: http://www.nmha.org/

Kuihusu: Shirika la Kitaifa la Afya ya Akili (NMHA) ndilo shirika nzee sana nchini na kubwa kabisa lisilo la faida linaloshughulikia hali zote za afya ya akili na ugonjwa wa akili. Likiwa na zaidi ya washirika 340 katika taifa lote. NMHA hufanyakazi ili kuboresha afya ya akili ya Waamerika wote, haswa watu milioni 54 walio na matatizo ya akili, kupitia utetezi, elimu, utafiti na huduma.

Jina: National Resource Center on Domestic Violence

Tovuti: http://www.nrcdv.org/

Kuihusu: Kituo cha Habari cha Kitaifa juu ya Mizozo ya Nyumbani (NRCDV) kilianzishwa mwaka wa 1993 kama sehemu muhimu ya mtandao wa kitaifa wa habari za Mizozo ya Nyumbani. NRCDV hutoa usaidizi kwa mashirika yote na watu wanaofanyakazi ya kumaliza mizozo katika maisha ya wahasiriwa na watoto wao kupitia usaidizi wa kiufundi, mafunzo na habari juu ya majibu ya uzuiaji mizozo ya nyumbani.

Jina: Recovery, Inc.

Tovuti: http://www.recovery-inc.org/

Recovery, Inc. ni mpango wa msaada wa kibinafsi wa afya ya akili ambayo msingi wake ni kazi nzito ya mwanzilishi wake, hayati Abraham A. Low, M.D., a neuropsychiatrist. mtaalamu wa tiba ya neva. Ni shirika liliso la kifaida, lisilo na kikundi na kinachosimamiwa kabisa na wanachama. Recovery Inc., limekuwa likifanyakazi tangu 1937 na lina mikutano ya vikundi kila wiki ulimwenguni kote.

Jina: Suicide and Mental Health Association International 

Tovuti: http://suicideandmentalhealthassociationinternational.org/

Kuihusu: SMHAI imejitolea kwa masuala ya kujiua na yanayohusiana na afya ya akili. Lengo lake kuu ni kuzuia tabia ya kujiua na kutoa athari zake kwa wale wote ambao wanawezakuwa wameathiriwa. Pia inakuza na kutetea elimu, ufahamu na tiba inayohusiana na afya ya akili.

Jina: World Association for Psychosocial Rehabilitation 

Tovuti: http://www.wapr.info/index.htm

Kuihusu: Shirika la Dunia la Kurekebisha Akili (WAPR) lilianzishwa nchini Ufaransa mnamo mwaka wa 1986 na limekuwa likiendelea sana tangu wakati huo. Kukua kwake katika miaka iliyopita kunaonyesha umuhimu unaoongezeka wa kuzuia na kupunguza ulemavu wa jamii kama mpangilio wa jamii kuwatunza watu walio na shida kali za akili.

Jina: World Federation for Mental Health

Tovuti: http://www.wfmh.org

Kuihusu: Shirika la Afya ya Akili Duniani lilianzishwa mnamo mwaka wa 1948 ili kuboresha kati ya watu wote na mataifa, uzuiaji wa matatizo ya akili na mhemko, matibabu na huduma halisi kwa wale walio na shida kama hizo, na ukuzaji wa afya ya akili

Jina: World Health Organization

Tovuti: http://www.who.int/en/

Kuihusu: Shirika la Afya Duniani ni chombo maalumu cha afya cha Umoja wa Mataifa

Jina: World Suicidology Net

Tovuti: http://www.redsuicidiologos.com.ar/           

 Kuihusu: Chanzo cha habari juu ya kujiua na masuala yanayohusiana.

Jina: World Wide Web Resources for Social Workers

Tovuti: http://www.nyu.edu/socialwork/ip/

Kuihusu: Kusaidia wataalamu wa huduma za jamii ulimwengu kote kudumisha vilivyo ufahamu wa habari kuhusu kazi hiyo na elimu ya bure inayotokea.