Breaking Through Barriers hulenga kusaidia kuhakikisha kwamba watu walio na unyogovu wanaosumbuliwa na dalili za mhemko na za kimwili wametambuliwa na kutibiwa vizuri kama iwezekanavyo Information for people with depression- Breaking Through Barriers hulenga kusaidia kuhakikisha kwamba watu walio na unyogovu wanaosumbuliwa na dalili za mhemko na za kimwili wametambuliwa na kutibiwa vizuri kama iwezekanavyo

Kujisikia nafuu

Kupanga mpango wa kupona

Kwa kuongezea kufanyakazi na daktari au mtaalamu mwingine wa huduma ya afya, mojawapo ya mambo mema unayoweza kufanya ni kubuni mpango wa kupona ili kusaidia kufikia malengo yako ya kupona.

Ijapokuwa Mwenza wako Msaidizi anaweza kukusaidia kukuza malengo yako na kukuhimiza njiani, ni jukumu lako kufafanua malengo yako na kuunda mafanikio ya kibinafsi.

Mpango kamili wa kupona:

Wakati wote wa kipindi cha ugonjwa wako, kunaweza kuwa na wakati dalili zako zinaendelea zaidi ) au umefikiria kujiua. Ukihisi dalili zozote za kuendelea zaidi kwa unyogovu, mawazo ya kujiua, mabadiliko yasiyo ya kawaidia kwa tabia zako, au wasiwasi, fadhaa, mishtuko ya hofu, ugumu wa kulala, kuwashwa, uhasama. uchokozi, mihemko, kutotulia, au kufurahi kupita kiasi na kuhangaika, unapaswa kuzungumza na daktari wako mara moja. Ikiwa moja kati ya mabadiliko haya ni kali au hufanyika kwa ghafula, inaweza kuonyesha hatari iliyoongezeka ya wazo au tabia yaa kujiua. Pia, kuwa mwangalifu sana uripoti dalili wakati wa kuanza tiba yoyote ya madawa ya unyogovu na wakati wowote kuna mabadiliko katika kipimo.

Kutunza shajara

Ni muhimu kwamba ufuate matibabu ambayo mtaalamu wa huduma ya afya aliyoagiza, na ufuate vile inavyoathiri dalili zako za mhemko na uchungu wa kimwili. Njia nzuri ya kufanya hivyo ni kutunza shajara inayojumuisha mizani ya kiwango cha mhemko cha 1– 10, ambayo ni muhimu sana. Ikiwa haujihisi kufanya hivyo, Mwenza wako Msaidizi anaweza kufanya hivi kwa ajili yako. Unaweza kuendelea baadaye, unapoanza kujihisi vyema.

Ikiwa unashiriki shajara yako na Mwenza wako, yeye anaweza kukuhimiza unapoanza kujihisi vyema au kuangalia ishara za kwamba dalili zako zinawezakuwa zinarudi. Fikiria kuhusu dalili za unyogovu wako wakati wewe au Mwenza wako anapoandika ndani ya shajara yako. Andika kidogo au kama utakavyo, lakini zingatia maelezo, kama vile:

Pia kumbuka kuandika unavyoendelea na maeneo ambayo unahisi unaendelea vyema, kama vile:

Ikiwa unatumia madawa ya unyogovu, angalia tena shajara yako baada ya kutumia madawa kwa wiki sita au zaidi. Kama vile mtaalamu wako wa huduma ya afya alivyokuambia, inaweza kuchukua wiki moja hadi nne au zaidi kwa madawa ya unyogovu kuanza kufanya kazi. Ikiwa haujihisi vizuri zaidi baada ya wiki sita hadi nane, unaweza kushiriki shajara yako na mtaalamu wako wa huduma ya afya na mjadili mabadiliko yoyote ya madawa yako. Ikiwa unaendelea na tiba, ni ya maana kwako kushiriki shajara yako na mtaalamu wako wa tiba pia.

Daktari wako atakuwa akiangalia kipimo na kuamua kama ni nzuri kwa kutibu dalili zote – za mhemko na za kimwili. Mtaalamu wa huduma ya afya atafafanua athari zinazoweza kutokea, ambayo ya kawaida sana inaweza kujumuisha kichefuchefu, kukauka mdogo, usingizi, hamu kupungua na kutoa jasho jingi. Athari zozote zisizotarajiwa zinapaswa kuripotiwa moja kwa moja kwa mtaalamu wa huduma ya afya.

Kuweka malengo

Unapoanza kujisikia vyema zaidi, ikiwa mtaalamu wako wa huduma ya afya atakubali, kuweka malengo inaweza kuwa sehemu muhimu ya kupona. Mwenza wako anaweza kukusaidia kuwaza kuhusu vitu ulivyokuwa ukifurahiya au ulivyokuwa ukivifanya vyema, na ungependa kufurahiya tena. Shiriki orodha yako na Mwenza wako, ili yeye aweze kukuhimiza unapoanza kufikia malengo yako.

Malengo haya yatakuwa ya kibinafsi sana kwako, lakini hapa kuna mawazo kadhaa ya kukuanzisha: Fuata mambo uliyokuwa ukifanya kabla ya kupata unyogovu Orodha hii si ya mambo ambayo umetaka kufanya au mambo ambayo haujawahi kufanya. Hapa kuna mifano kadhaa:

Kujijali

Hauwezi kukimbia mbio za masafa marefu baada kupasuliwa goti. Kupona kutoka kwa unyogovu siyo tofauti vile – unahitaji muda wa kupona na kujisikia nafuu. Kumbuka, Mwenza wako Msaidizi yuko hapo ili kukuangalia, lakini pia unapaswa kujishughulikia vizuri sana. Jijali kwa kula vizuri, kupumzika vya kutosha na kushughulika na kutembea nje au zoezi lolote ambalo unahisi ni sawa kwako. Jaribu kujifanyia chochote kinachofunya ujihisi vizuri na uchukue muda wa kutulia na kupumzika.