Kupata usaidizi: Kuimarisha ubia
Kujifunza pamoja kuhusu unyogovu
Unapokuwa ukizungumza kwa uaminifu na Mwenza wako Msaidizi kuhusu hisia zako, unaweza kukabiliana na kutoelewana au mawazo mabaya. Ni muhimu kwa kila mtu anayehusika kukumbuka kwamba unyogovu ni ugonjwa wa akili na mwili – si sawa na “kuhisi kutochangamka” na siyo jambo unaloweza kutaka liende. Kuna njia nyingi kwako na Mwenza wako Msaidizi kujifunza kuhusu ugonjwa wako. Kwa habari zaidi, enda kwa sehemu ya tovuti hii ya Kuelewa Unyogovu Pia, utataka kuzingatia Mwenza wako Msaidizi ahudhurie miadi kati yako na mtaalamu wa huduma ya afya. Hii itampa Mwenza wako nafasi ya kupata ushauri muhimu wa njia bora ya kukusaidia, au kujadili hofu yoyote au hoja.
Mwenza wako Msaidizi anawezaje kukusaidia?
Kwa kuwa sasa umeanza mazungumzo na Mwenza wako Msaidizi kuhusu unyogovu wako, ni muhimu kuamua vile anavyoweza kukusaidia vilivyo. Kwa kuwa tayari umefikiria kuhusu aina ya usaidizi unaohitaji — ya kikazi na ya mhemko — unastahili kuwa wazi kuhusu mahitaji yako. Kuwa mahsusi sana kuhusu mambo ambayo ungependa kusaidiwa na mambo ambayo unaweza kufanya vizuri kivyako. Hii itakuwa ya msaada kwa Mwenza wako na itaweka mipaka wazi kwa ubia wako wa usoni. Hapa kuna mifano kadhaa ya usaidizi wa mhemko na wa kazi.
Usaidizi wa Mhemko:
- Kupiga simu kila jioni ili kuniangalia
- Kupatana mara moja kwa wiki
- Kunisaidia kufahamu mambo ambayo yanaweza kunifanya unyoguvu wangu uzidi
- Kunihimiza nifuate matibabu
- Kunisaidia kutambua ninavyoendelea
- Kunisaidia kuweka malengo ya kweli ya muda mfupi, ikiwa imependekezwa na mtaalamu wangu wa tiba
- Kunihimiza nishughulike kama iwezekanavyo
Usaidizi wa Kikazi:
- Kufanya miadi na mtaalamu wa huduma ya afya
- Kuwachukua watoto kutoka shuleni au shughuli za baada ya shule
- Kusaidia na makaratasi ya huduma ya afya
- Kupika chakula cha jioni mara moja kwa wiki
- Kunipeleka kwa miadi ya madaktari
- Kutekeleza safari fupi
- Kupanga muda wa kutembea au kwenda mazoezi pamoja
- Kuweka tarehe ya kwenda kuona sinema
Kuweka malengo ya usoni
Kwa muda, kuwa na Mwenza Msaidizi wa kukusaidia itakuwa usaidizi mkubwa na itakuruhusu kuzingatia kupona. Walakini, baada ya muda mrefu, wewe na Mwenza wako mnastahili mpange mpango ambao utakusaidia kuchukua kazi hizi polepole. Kufanyakazi kuelekea na kufikia kila lengo itakusaidia kujisikia nafuu.
