Kupata usaidizi: Kuuliza usaidizi
Kwa kuwa sasa umemtambua mtu anayeweza kuwa Mwenza Msaidizi, ni wakati wa kuuliza usaidizi. Ukweli ni kwamba, sisi wote tunahitaji usaidizi mdogo kila wakati. Unaweza kushangazwa kujua kwamba watu wengi unaowajua watafurahiya kukusaidia — au kwamba wanaweza kuwa wamepitia hali kama hiyo au wanawajua wengine ambao wamepitia hali hiyo. Kumbuka, unyogovu ni ugonjwa ambao unaweza kuzidi ukikosa matibabu kamili na usaidizi wa familia au marafiki.
Jinsi ya kuuliza usaidizi
Ikiwa hauna uhakika wa jinsi ya kuanza, hapa kuna vyanzo kadhaa rahisi vya mazungumzo unavyoweza kupata kuwa ni vya msaada:
- “Unajua … nimechoka kuhisi kutochangamka kila wakati. nilipata mtaalamu wa huduma ya afya ambaye ananisaidia kuishi maisha ninayotaka. ningependa kukueleza kuyahusu...”
- “Kama watu wengine wengi, nina siku za kutochangamka, lakini ninajifunza kwamba nina unyogovu na ninahitaji kufanya bidii kuhusu kupona kwangu zaidi ya wengine…”
- “Ninafikiria kwenda kumuona daktari kuhusu kuumwa na uchungu ambao nimekuwa nao hivi karibuni. sijihisi ni kama niko sawa, na ningependa kukueleza kuyahusu …”
- “Ninajihisi mpweke sana na niliyejawa na mhemko siku hizi. ninafikiria ninamwitaji mtu wa kuzungumza na yeye …”
- “Ninajua uhusiano wetu haujakuwa sawa siku hizi na …”
- “Daktari wangu anasema nina unyoguvu. Ninapata matibabu ya kunisaidia kuhisi vyema, lakini ninadhania kwa sasa ninahitaji usaidizi …”
Je! mtu akisema “hapana?”
Kwa sababu ya shinikizo ya kikazi, ya kifamilia au ya juhudi zingine, rafiki au mpendwa anaweza kukosa kukupa wakati unaohitaji, au wanaweza kuhisi kwamba wanastahili kujitolea ili kuwa Mwenza mzuri. Hii haionyeshi ukosefu wa kujali au uhusiano dhaifu, kwa urahisi inamaanisha hawezi kujitolea hivi sasa. Shukuru kwa uaminifu kama ishara ya heshima kwako na uelewe kwamba ilikuwa vigumu sana kusema “hapana”.
Weka akilini, hatuwezi kujua kila kitu kuhusu maisha ya yule mwingine; inawezekana kwamba rafiki yako anangangana na masuala yake ya kibinafsi. Kuwa mpole na yeye na uweke wazi mlango wa uhusiano baadaye wakati mambo yako sawa kwenyu wote. Kama hatua inayofuata, rejea kwa orodha yako ya watu wanaoweza kuwa Wenza Wasaidizi ili umtambue mtu mwingine.
