Breaking Through Barriers hulenga kusaidia kuhakikisha kwamba watu walio na unyogovu wanaosumbuliwa na dalili za mhemko na za kimwili wametambuliwa na kutibiwa vizuri kama iwezekanavyo Information for people with depression- Breaking Through Barriers hulenga kusaidia kuhakikisha kwamba watu walio na unyogovu wanaosumbuliwa na dalili za mhemko na za kimwili wametambuliwa na kutibiwa vizuri kama iwezekanavyo

Kupata usaidizi: Kumchagua Mwenza

Je! Mwenza Msaidizi ni nani?

Mwenza Msaidizi ni mtu ambaye amejitolea kukusaidia uwe sawa. Mtu huyu anaweza kutoa himizo inayohitajika ili kukusaidia kuamini kwamba unyogovu unaweza kushindwa. Usaidizi unaweza kutolewa kwa njia nyingi tofauti na watu wengi tofauti, ikitegemea na mahitaji yako ya kibinafsi. Watu wengine walio na unyogovu wanaweza kuhitaji Mwenza Msaidizi ili kutoa mahali salama pa kujadili jitihada, ushindi na vikwazo vya unyogovu, wakati wengine wanaweza kutafuta isaidizi wa kazi za kila siku. Mtu yeyote anaweza kuwa Mwenza Msaidizi – washirika wa familia, marafiki, wafanyakazi wasaidizi, waalimu, majirani, vikundi vya usaidizi na wengine.

Unaweza kupata ni vigumu kukubali usaidizi mara ya kwanza kwa sababu nyingi - aibu, ukosefu wa ufahamu kuhusu unyogovu, hisia za kutokuwa na dhamana au uwoga wa kupoteza uhuru. Hii ikifanyika, usiwe na wasiwasi. Wakati haujafika wa kukubali usaidizi. Lakini kumbuka, kuna watu unaweza kutafuta usaidizi kutoka kwao; inakubidi tu ukubali usaidizi wao wakati muda utakapofika.

Uwezo wa usaidizi

Kuuliza mkono wa usaidizi au mbega ya kuegemea haipaswi kukufanya uhisi haya au aibu. Inamaanisha kwamba unafanya kazi kwa bidii ili kupona. kwa kweli, kuwa na Mwenza itakupatia manufaa mengi. Mwenza Msaidizi anaweza:

Kumpata Mwenza Msaidizi mzuri kabisa kwa ajili yako

Kabla ya kumuuliza mtu usaidizi, andika chini orodha ya kila mtu ambaye una uhusiano na yeye – watu ambao unawaamini, ambao ni watulivu na wanaoelewa na wale ambao hawatakuhukumu. Tayari unaweza kuwa una mtu akilini ambaye atakuwa Mwenza wako, lakini ikiwa hauwezi kufikiria kuhusu mtu yeyote kwa sasa, orodha hii inaweza kuduguda kumbukumbu yako. Ukiamua kuwa ungependelea kuwa na zaidi ya Mwenza Msaidizi mmoja, orodha hii inaweza kukusaidia kufikiria watu ambao unataka kufanyakazi nao. Kumbuka, ijapokuwa ni muhimu kuwa na Mwenza Msaidizi katika maisha yako, yeye hastahili kubadilisha mahitaji ya matibabu ya mtaaalamu wa huduma ya afya aliyehitimu.

Mambo ya kuzingatia kabla ya kuchagua

Kwa kuwa sasa una wazo la yule katika maisha yako anaweza kuwa Mwenza mzuri, unaweza kuanza kufikiria kuhusu aina ya usaidizi unaohitaji. Iwe unahitaji usaidizi wa mhemko au wa kikazi, kufikiria kuhusu unachohitaji itakusaidia kuchagua Mwenza anayestahili. Pia, ni muhimu kuwa na uhakika kwamba umemchagua mtu ambaye hana shughuli nyingi sana na yule ambaye hasafiri mara kwa mara kwa ajili ya kazi yake. Ikiwa hauna uhakika kuhusu aina ya usaidizi unaohitaji, jiulize mwenyewe maswali yanayofuata:

Ikiwa umejibu “ndiyo” kwa mengi ya maswali haya, unahitaji Mwenza Msaidizi ambaye anaweza kutoa usaidizi wa kikazi wa safari fupi au utunzaji nyumba.

Ikiwa umejibu “ndiyo” kwa mengi ya maswali haya, unamwitaji Mwenza ambaye anaweza kuwa hapo kwa ajili yako kihisia.