Kutafuta usaidizi wa kimatibabu
Unyogovu ambao haujatambuliwa unaweza kuwa mbaya sana – utafiti wa kimatibabu unaonyesha kwamba, vile mtu aliye na unyogovu anavyoendelea bila kutibiwa, ndivyo hali yake inadumu zaidi na ndivyo nafasi yake ya kupona kabisa inaenda chini1. Ikiwa tayari haujafanya hivyo, wasiliana na mtaalamu wa kimatibabu aliyehitimu kwa haraka iwezekanavyo.
Kama hatua ya kwanza, zungumza na daktari wako asili kuhusu chaguzi zako, ambazo zinaweza kujumuisha mtaalamu wa tiba na magonjwa ya akili, mwanasaikolojia, mshauri aliyeidhinishwa wa afya ya akili au mfanyakazi wa jamii wa taaluma ya tiba na magonjwa ya akili. Madaktari wengi asili wako sawa na kuwatibu watu walio na unyogovu. Mtaalamu wa tiba na magonjwa ya akili ni daktari ambaye anaweza kuagiza madawa na ni mtaalamu wa kutibu magonjwa ya akili kama vile unyogovu. Mwanasaikolojia si daktari, na kwa hivyo hawezi kuagiza madawa; mwanasaikolojia ni mtaalamu wa tiba ya kuzungumza. Kwa njia zingine za kupata mtaalamu wa huduma ya afya aliyehitimu, tafadhali rejea sehemu ya Rasilimali na Viungo.
Kupata huduma nzuri ya matibabu ni muhimu na inaweza kuongeza nafasi ya mtu ya kuwa sawa. Kabla ya kufanya miadi na mtaalamu wa huduma ya afya, inaweza kuwa ya msaada kuandika chini maswali ambayo ungependa mtaalamu wa huduma ya afya ajibu; kuja na orodha hiyo kwa miadi. Kwa mfano, zingatia kuuliza:
- Je! una ujuzi wa kutibu unyogovu?
- Unatibu aje unyogovu?
- Unawahusisha aje familia au marafiki kwa matibabu?
- Je! ni mara ngapi ninapaswa kusema, na unaweza kufikiwa aje wakati wa hali ya dharura?
- Je! unaweza kuagiza madawa?
Mtaalamu wako wa huduma ya afya anaweza kujibu maswali yoyote unayoweza kuwa nayo kuhusu unyogovu na matibabu, hata pia kutoa ushauri kwa wale ambao wanataka kusaidia. Hapa kuna maoni kadhaa:
- Je! matibabu yatashughulikia dalili zangu zote — mhemko na kimwili?
- Je! madawa yanaweza kubadilisha utu wangu?
- Nitajua aje kama tiba ya kuzungumza inafanya kazi?
- Je! kuna hatari zozote za kutumia madawa?
- Je! nitazizoea?
- Je! Athari gani mbaya ninapaswa kuangalia?
- Je! nifanye nini nikizipitia?
- Je! Ni ishara gani ya kuwa tiba inafanya kazi na ninaweza kufanya nini ikiwa tiba haionekani kufanya kazi?
- je! Nitaanza lini kujihisi vyema?
- Je! Ni lazima nitumie madawa maisha yangu yote, au ninaweza kuwacha kuzitumia nikihisi vyema?
- Je! Unyogovu huo utarudi tena?
Rejeleo
- 'Depression: The Painful Truth' Survey. Conducted by Harris Interactive between February 21 and April 11, 2005. Inapatikana kwa: http://www.wfmh.org/PainfulTruthsurvey.htm
