Kuelewa unyogovu
Kila mtu uhuzunika au kupoteza tamaa ya vitu wakati mwingine. Ijapokuwa, watu walio na unyogovu, hisia hizo zinaweza kudumu kwa wiki au miezi na ikiwachwa bila kutibiwa, inaweza kudumu kwa miaka. Unyogovu si kwa sababu ya mtu yeyote - wala mwenye kusumbuka au mtu yeyote katika maisha yake. Badala yake, ni hali ya kimatibabu ambayo, kama magonywa mengine, inaweza kutibiwa kutibiwa. Jambo muhimu ni kutafuta usaidizi.
Unyogovu unaweza kujumuisha aina mbalimbali za dalili za mhemko na za kimwili ambazo zinatofautiana kutoka kwa mtu hadi mwingine. Madaktari wanaamini mambo mengi tofauti yanaweza kusababisha unyogovu, kutoka kwa matukio ya maisha hadi mabadiliko ya kimwili mwilini. Mambo haya hufanya iwe changamoto kugundua dalili ndani yako au mtu unayempenda na kutafuta usaidizi.
Ikiwa unadhania kwamba wewe au mtu unayemjua anaweza kuwa na unyogovu, jifunze kabisa kama uwezavyo kuhusu hali hiyo. Kuelewa unyogovu ni nini - na siyo nini - ndiyo hatua ya kwanza ya kupata usaidizi.
