Mwito wa kuchukua Hatua: Kukuza Ufahamu na Kuboresha Utambuzi wa Unyogovu
Matokeo ya kutisha ya Utafiti wa ‘Unyogovu: Ukweli wa Kuhuzunisha’ , ilifanya Shirikisho la Afya ya Akili Duniani (WFMH) kuita mkutano wa wataalamu kutoka maeneo tofauti ya taaluma na tiba ya magonjwa ya akili - madaktari wanaoongoza na mawakili wa wagonjwa - katika majira ya joto ya 2005 ili kujadili njia mpya za kuboresha utambuzi wa unyogovu na kuongeza ufahamu wa ugonjwa huo. Mkutano huu ulidhaminiwa na Eli Lilly and Company na Boehringer Ingelheim.
Wataalamu hawa walihakiki uchunguzi wa sasa na utafiti wa hivi karibuni, na wakashiriki maoni yao ya hospitali na ya maeneo ili kuanzisha taarifa ya makubaliano na mpango wa hatua iliyoundwa ili kushughulikia mahitaji ambayo hayajafikiwa ya unyogovu na kuboresha maisha ya watu walio na unyogovu ulimwenguni kote.
Vipengele muhimu vya makubaliano
- Ni muhimu kuongeza ufahamu wa dalili zote za unyogovu kwa umma, pamoja na dalili za uchungu wa kimwili zinazohusiana na unyogovu ili kuwahimiza watu walioambukizwa kutafuta usaidizi wa mtaalamu mapema na kuwasaidia kuonyesha dalili zao kwa daktari wao wa asili.
- Ni muhimu kuboresha elimu ambayo madaktari asili wanapokea kuhusu unyogovu, haswa katika shule za utabibu, ili kusaidia kuhakikisha kwamba wanatambua unyogovu kwa usahihi. Hii itahakikisha watu walio na unyogovu watatathminiwa, wakizungumza na madaktari wao kuhusu dalili za uchungu unaoendelea bila sababu ya kimatibabu.
Kikundi cha wataalamu pia kiliitwa kwa mambo maalum ya kuchukua hatua mnamo 2006, pamoja na uanzishaji wa Tovuti; kuleta pamoja vikundi vya kimataifa vya kuwatetea wagonjwa ili kujadili mipango ya kushughulikia vipengele vya makubaliano; kudhamini warsha ya ‘mazungumzo binafsi ya Unyogovu’ ya vyombo vya habari ili kuangazia athari ambayo unyogovu inayo kwa wanawake; na kutekeleza utafiti wa kuelewa vyema na kuangazia mapengo kati ya elimu ya unyogovu na kazi ya hospitali.
Mwito wa kuchukua Hatua umekubaliwa na majopo yafwatayo ya wataalamu wa kimataifa:s
- Prof. Michael Bauer (Charité – University Medicine Berlin, Germany)
- Gabriela Camara (Voz Pro Salud Mental, Mexico)
- Dr. Adriano Camargo (ABRATA, Brazil)
- Dr. Ricardo Colin (Instituto Nacional de Neurologia y Neurocirugia, Mexico)
- Dr. Vincenzo Costigliola (European Medical Association, Belgium)
- Dr. Marc-Antoine Crocq (Centre Hospitalier de Rouffach, France)
- Prof. Pedro Delgado (University of Texas, USA)
- Dr. Patt Franciosi (World Federation for Mental Health)
- Preston Garrison (World Federation for Mental Health)
- Margit Golfels (TriaLogisch e.V. / Hilfe für psychisch Kranke Bonn/Rhein-Sieg e.V., etc., Germany)
- Amelia Mustapha (European Depression Association)
- Prof. Robert Peveler (University of Southampton, UK)
