Utafiti wa ‘Unyogovu: Ukweli wa Kuhuzunisha.’
Shirikisho la Afya ya Akili Duniani (WFMH), liliitisha utafiti wa ‘Unyogovu: Ukweli wa Kuhuzunisha’ mnamo mwaka wa 2005 ili kupima vile madaktari na watu walio na unyogovu wanavyofahamu uunganisho kati ya dalili za unyogovu wa mhemko na uchungu wa kimwili, na kutambua utambuzi unaowezekana na mapengo ya matibabu 1. The (WFMH) imejitolea kuboresha ulezi na ahueni ya watu walio na matatizo ya kiakili, pamoja na watu wale wanaosumbuliwa na unyogovu.
Mapato kutoka kwa utafiti wa kimataifa ulionyesha kwamba watu walio na shida kubwa ya unyogovu, kwa kadri, walisubiri miezi 11 ili kumwona daktari kuhusu dalili zao1. Hata wakati huo, walitambuliwa walikuwa na unyogovu baada ya kumtembelea daktari mara tano, hii ilichelewesha zaidi matibabu na ahueni1. Utafiti huu pia ulifichua kwamba hata baada ya kutambuliwa, asilimia 72 ya watu walio na shida kubwa ya unyogovu hawakugundua kwamba dalili za uchungu wa kimwili, kama vile kuumwa na kichwa bila sababu, kuumwa na mgongo, matatizo ya mmengenyo wa chakula na kuumwa na uchungu bila sababu, zilikuwa dalili za kawaida za unyogovu1. Walakini, asilimia 79 ilikubali kwamba dalili hizi zilisumbua au zilisumbua sana, na kwamba dalili hizi ziliwasababisha wamuone daktari na unyogovu kutambuliwa1 .

Kwa matokeo ya kina zaidi ya utafiti, angalia Utafiti wa ‘Unyogovu: Ukweli wa Kuhuzunisha’
Kwa sababu matokeo ya utafiti yalikuwa yakitatanisha sana, jopo la washauri wataalamu waliitwa ili kubuni mpango wa Breaking Through Barriers program.
- ‘Depression: The Painful Truth’ Survey. Ilifanywa na Harris Interactive kati ya Februari 21 na Aprili 11, 2005. Inapatikana kwa: http://www.wfmh.org/PainfulTruthsurvey.htm
