Kuhusu Breaking Through Barriers

Kwa kuwaelimisha watu walio na unyogovu, watoa huduma ya ulezi, na madaktari na kuboresha mawasiliano kati ya mgonjwa na daktari, Breaking Through Barriers hulenga kusaidia kuhakikisha kwamba watu wenye unyogovu wametambuliwa na kutibiwa vizuri kama iwezekanavyo na kupunguza hisia ya aibu ambayo watu wengi walio na unyogovu bado wanayo.

Mpango huu ulitoka kwa Utafiti wa Unyogovu: Ukweli wa Kuhuzunisha , utafiti wa kimataifa uliotekelezwa kwa niaba ya Shirikisho la Afya ya Akali Duniani (WFMH) mapema mwaka wa 2005 1. Utafiti huo ulifichua mapengo makubwa ya ufahamu wa wagonjwa' na madaktari' kuhusu unyogovu na ilionyesha vile mapengo haya yanasababisha utambuzi mbaya au utambuzi uliyocheleweshw1.

Baada ya kushtuliwa na matokeo hayo, WFMH iliwaleta pamoja wataalumu wanaongoza ili kujadili njia za kuboresha ufahamu na utambuzi wa unyogovu. Mawazo yao, yaliyosemwa kwa muhtasari wa Mwito wa kuchukua Hatua , ilisababisha uanzishaji wa mpango wa Breaking Through Barriers na Tovuti hii

Ili kuhakikisha kwamba Breaking Through Barriers inafikia viwango vya juu kabisa, kamati ya wahakiki inayojumuisha madaktari na wakilishi wa kikundi cha kuwatetea wagonjwa uhakiki nyenzo zote za mpango.

Breaking Through Barriers imedhaminiwa (WFMH), Eli Lilly and Company na Boehringer Ingelheim, na inasaidiwa na mashirika ya wagonjwa na madaktari wanaoongoza kila mahali Uropa na Amerika ya Kusini.

Rejeleo
  1. ‘Depression: The Painful Truth’ Survey.  . Ilifanywa na Harris Interactive kati ya Februari 21 na Aprili 11, 2005. Inapatikana kwa: http://www.wfmh.org/PainfulTruthsurvey.htm